SHIRIKA la Walimu wa Elimu ya Mahitaji Maalum (OSNET) linatoa fursa kwa Shule za Msingi na Sekondari Nchini Tanzania (zenye wanafunzi wenye ulemavu na wasio na ulemavu) kutuma maombi ya kushiriki katika shindano la Ubunifu wa Shule.
The Organization of Special Needs Education Teachers (OSNET) is giving an opportunity to Primary and Secondary Schools Inclusive in Tanzania (with students with and without disabilities) to apply to participate in the School Innovative Challenge
Kumbuka: Hakikisha wazo ni la kipekee na lenye tija kwa maisha endelevu ya wanafunzi.
Note: Make sure the idea is unique and productive for the sustainable life of the students.
Kupitia fomu hii, Walimu kwa kushirikiana na wanafunzi wao katika klabu za Elimu maalum watajaza mapendekezo yao 1 – 5 wanayotegemea kuyatekeleza.
Through this form, teachers in collaboration with their students in special education clubs will fill in their suggestions 1 – 5 that they plan to implement.
Shule zitakazoibuka katika mchujo zitapatiwa semina wezeshi, vifaa na ruzuku itakayosaidia kumudu mahitaji ya utekelezaji wa wazo.
The schools that will emerge in the selection will be provided with facilitating seminars, equipment and grants that will help to meet the needs of the implementation of the idea.
Hata hivyo, Baada ya upimaji wa utekelezaji wa mawazo hayo, Shule 3 zitakzaoibuka bora zitapatiwa zawadi kwa ajili ya uendelezaji wa vipawa vyaa wanafunzi ikiwemo vyeti vya ushiriki na fedha taslimu.
However, after evaluating the implementation of these ideas, the 3 best schools will be awarded for sustaining students’ talents, including certificates of participation and cash
Muda (Duration):
Maombi yataanza tarehe 26 Septemba 2023 hadi 4 Oktoba 2023
Applications will start from 26 September 2023 to 4 October 2023
Usaili wa upitiaji wa maombi utafanyika tarehe 6 Oktba 2023. Orodha ya shule zitakazopitisha katika mchakato huu itatolewa tarehe 8 Oktoba 2023.
The review of applications will take place on October 6, 2023. The list of schools that will pass through this process will be released on October 8, 2023.
Utoaji wa taarifa (Provision of information)
Taarifa zote kuhusu program hii zitatolewa kwa njia ya group la OSNET Network ya WhatsApp, tovuti, barua pepe na kwenye mitandao ya kijamii.
All information about this program will be provided through the OSNET Network WhatsApp group, website, e-mail and on social networks.
You can either fill out this form online or offline. Offline forms must be scanned and sent back to Osnet before the deadline.